| MKATABA WA UPANGISHAJI |
MAKUBALIANO HAYA YAMEFANYIKA siku ya tarehe ya mwezi wa mwaka 20..
BAINA YA ’
Ndugu ................................ wa sanduku la barua .........., ambaye ndani ya mkataba huu atakua anatajwa kama MPANGISHAJI
NA
Ndugu ..................... wa sanduku la barua ................, ambaye ndani ya mkataba huu atakua anatajwa kama MPANGAJI
KWA KUWA:
a) MPANGISHAJI ndiye, na ataendelea kuwa mmiliki halali wa chumba cha biashara kilichopo............, chumba ambacho ndani ya mkataba huu kinatajwa kama chumba cha biashara
b) Na kwamba MPANGISHAJI ana hiaari, kwa kuzingatia kufuatwa kwa masharti yanayoainishw kwenye mkataba huu, ya kumpangisha MPANGAJI chumba cha biashara kwa ajili ya kufanyia biashara halali;
c) na kuwa MPANGAJI, kwa hiari yake, yuko tayari kupanga chumba hicho kinacho pangishwa kwa kufuata, na bila kuvunja masharti yanayoainishwa katika mkataba huu;
WAHUSIKA WA MKATABA HUU WANAKUBALIANA YAFUATAYO:
a. KWAMBA, kwa malipo ya KODI inayoainishwa katika mkataba huu, na kulingana na masharti ya upangaji kama yanavyainishwa katika mkataba huu, MPANGISHAJI anaipangisha chumba cha biashara kwa MPANGAJI;
b. NA KWAMBA MPANGAJI atalipa Shilingi .............(Shilingi ..............) kwa mkupuo kwa MPANGISHAJI, malipo ambayo ni KODI ya miaka miwili kwa kiwango cha shilingi .................kwa mwezi;
c. NA KWAMBA mkataba huu umeanza kutumika Siku ya tarehe....mwezi wa ..., mwaka ambapo MPANGAJI atarushusiwa kutumia chumba cha biashara;
KWA MASHARTI YAFUATAYO:
a Endapo
(i) katika kipindi cha upangaji kodi haitokua imelipwa kwa muda wa siku ishirini na moja na / au
(ii) MPANGAJI, bila sababu ya msingi, akashindwa kuzingatia masharti muhimu ya upangishaji, katika mkataba hu;[1]
Itakua ni halali kwa mpangishaji, kutwaa chumba cha biashara;
b) Taarifa (NOTICE) inayohusiana upangaji katika mkataba huu itakua ni kwa njia ya maandishi;
c) Mkatabaa huu unaweza ukarefushwa kulingana na makubaliano wa wahusika wote wawili. Katika kipindi chote cha kupitia upya na kurefushwa kwake, kiasi cha kodi kitajadiliwa upya kulingana na mazingira ya kibiashara kwa wakati huo;
d) MPANGAJI anaweza akavunja mkataba kabla ya kumalizika kwa kipindi chake, baada ya kutoa taarifa kwa MPANGISHAJI: lakini kwa hali yoyota, uvunjaji wa mkataba ndani ya kifungu hiki hautoruhusu kurudishwa kwa KODI itakayokua imeshalipwa.
KWA MASHARTI HAYO, MPANGAJI ANAKUBALI YAFUATAYO:
1. Kulipa KODI kwa kwa kiasi kinachotajwa katika mkataba huu;
2. Kulipa Gharama za uafi, maji na umeme kwa mamlaka husika;
3. Kwa wakati wote, kuweka chumba cha biashara katika hali bora, na usafi kwa matumizi ya biashara;
4. Kuruhusu MPANGISHAJI au mtu yeyote kwa niaba yake, kuingia na kufanya matengenezo au ukaguzi unaohusiana na ubora wa chumba cha biashara;
5. Kutofanya upanuzi, au kubadilisha sehemu yoyote ya chumba cha biashara bila ridhaa ya MPANGISHAJI;
6. Kutompangisha mtu yoyote bila ridhaa ya MPANGISHAJI;
7. kutotumia chumba cha biashara kwa hali yoyote ambayo itasababisha kero au usumbufu kwa majirani au wafanyabiashara wengine;
8. Kutumia chumba cha biashara kwa madhumuni ya biashara tu;
9. Kwamba Biashara itakayofanyika isiwe ni kinyume cha shsria za nchi;
10. Kwamba MPANGAJI atawajibika kwa uharibifu wa makusudi au uzembe, katika chumba cha biashara;
11. Wakati mkataba utakapofikia ukingoni, na kabla ya kurefushwa kwake, MPANGAJI atakabidhi chumba cha biashara kikiwa katika hali nzuri ya kibiashara.
NA MPANGISHAJI ANAKUBALI YAFUATAYO:
1. Kuhakikisha kwamba MPANGAJI hatopata usumbufu wowote, na kwamba baada ya MPANGAJI kulipa KODI na kutimiza masharti yote ya UPANGANI, MPANGISHAJI atakua huru kutumia chumba cha biashara kwa ajili ya madhumuni yanayoainishwa katika mkataba huu bila ya vikwazo vyovyote ambavyo ni kinyume na mkataba;
2. Kukifanyia matengenezo chumba cha biashara, na kuhakikisha kwamba wakati wote kiko katika hali nzuri kwa ajili ya biashara, pale ambapo hali itakayopelekea kuhitajika kwa matengenezo haitokuwa ni kwa ajili ya matendo ya MPANGAJI, kwa makusudi au uzembe, yatakayosababisha uharibifu;
3. Kulipa malipo yote katika mamlaka husika, malipo ambayo MPANGAJI hajatajwa kuhusika nayo katika mkataba huu.
MBALE YA MASHAHIDI, MPANGAJI amemlipa MPANGISHAJI kiasi cha Shilingi za Kitanzania kama KODI kwa kipindi cha miaka miwili;
NA INASHUHUDIWA kwamba wahusika katika mkataba huu wameingia mkataba huu siku hii ya kama inavyo onekana hapo chini:
………………………. ambaye
Ninamfahamu katika siku hii ya
tarehe mwezi wa 2011 MPANGHISHAJI
MBELE YANGU
Sahihi:
Jina
Anuanii:
………………………….
ambaye ninamfahamu katika siku hii ya
tarehe mwezi wa 2011 MPANGAJI
MBELE YANGU
Sahihi:
Jina
Anuanii:
[1] Masharti Muhimu ya upangishaji ni yale yanayo husiana na utunzaji wa chumba cha biashara, na malipo ya kodi.




7 comments:
Asanthe sana, Umeniokoa kwenye aibu
Many thanks!
Much thanks mkuu, umenisaidia sana
Asante sana
Ahsante sana, Kwa ruhusa yako mwandishi naomba niutumie huu mkataba mahali fulani.
ASANTHE SANA KWA MKATABA HUU BORA
Unaweza nisaidia mkataba wa kufundisha kama nina wanafunzi wangu mawafundisha cherehani nataka niandae mkataba tafadhari
Post a Comment