MKATABA WA AJIRA YA MUDA


MKATABA WA AJIRA YA MUDA

MKATABA HUU unafanyika leo tarehe ………… mwezi …………………., 2011.

BAINA YA


……………….., wa S.L.P ………………… (ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama “Mwajiri”) wa upande mmoja wapo wa Mkataba

NA


……………………………. S.L.P ………………….. (ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama “Mwajiriwa”)

AMBAPO


a)            Mwajiri ni Kampuni iliyopo Dar es Salaam inayoshughulika na Matangazo ya Biashara.

b)            Mwajiriwa anafanya Shughuli Binafsi Dar es Salaam.

c)            Mwajiri anakusudia kumwajiri kwa muda Mwajiriwa

Mwajiriwa anakubali matakwa ya mwajiri na anakubali kwa hiari yake mwenyewe kuajiriwa kwa muda kama MSANII/MHAMASISHAJI/DJ WA MRADI.

MKATABA HUU UNASHUHUDIA haya yafuatayo

i.              Mwajiriwa atawajibika kufanya kila jambo ambalo ujumla wake atahakikisha mafanikio ya mradi wa………………….atakaoendeshwa kwa muda wa…………………….…………..kuanzia tarehe ………………………………….
ii.            Mwajiriwa atatarajiwa kuonekana nadhifu kama Msanii/DJ/Mhamasishaji katika kipindi chote cha kazi hii.
iii.           Mwajiriwa atatakiwa kuripoti kazini saa ……………………….   tayari kwa matayarisho ya shughuli zake za siku na ataanza kazi saa ………………, (Muda wa kuanza na kumaliza kazi unaweza kubadilika kufuatia utashi wa mteja).
iv.           Mwajiriwa atatakiwa kuwajibika katika kuandaa vyema kituo chake cha kazi, steji, gari au vifaa vya kazi kwa unadhifu mkubwa.
v.            Mwajiriwa atahakikisha anao ufahamu wa kutosha wa kile anachotakiwa kupromoti.  kufanya maandalizi ya vifaa vitakavyokuwezesha kutekeleza malengo ya kazi husika  kama vile vipeperushi, spika n.k.
vi.           Mwajiriwa atafanya maonesho kwa umakini na umahiri mkubwa ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wananufaika na juhudi zako.
vii.          Mwajiriwa atatawajibika kwa Mkuu wa kazi (Project Manager/Promoter) kwa utendaji wake wa kila siku.
viii.        Mwajiriwa atalipwa jumla ya kiasi cha Tshs………………………… atakapofanikisha shughuli za mradi huu ambao utachukua muda wa siku  …………………
ix.           Mwajiriwa atatakiwa kuhudhuria mikutano ya tathmini pamoja na Watendaji wengine wa timu yako kila siku/wiki.
x.            Ili kuhakikisha mafanikio Mwajiriwa atatakiwa kutekeleza maelekezo ya kiongozi wako wa mradi.
xi.           Ambapo promosheni inapaswa kuanza kwa muda uliopangwa na ucheleweshaji wa jambo lolote linalohusiana na promosheni hautavumiliwa au kukubaliwa.
xii.          Kwamba atapata malipo yake wiki mbili (2) baada ya kukamilika kwa mradi.  Katika muda huo inatarajiwa kuwa taarifa zote zitakuwa zimekamilishwa  na kuwasilishwa, marejesho ya vifaa vyote vya kazi na fedha za mradi yatakuwa yamefanyika.
xiii.        Ifahamike kwamba utoaji wa siri za Kampuni ya Dunia na wizi ni mambo ambayo sio tu hayaruhusiwi lakini pia hayatavumiliwa.
xiv.        Kwamba Kampuni ya Dunia inauwezo wa kubadilisha baadhi ya masharti haya na hata kusitisha Mkataba nawe wakati wowote.
xv.          Masharti ya nyongeza mahsusi kuhusiana na mradi huu ni pamoja na:-………………………………………………………….. …………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………

KWA USHUHUDA HUU, pande zote mbili zinaweka sahihi zao katika Mkataba huu siku na tarehe kama ilivyo hapa chini.



Imesainiwa Dar es Salaam na
………………………………….                   …………………………………
Kwa niaba ya ……………
………… leo tarehe …………..
Mwezi …………………, 2011.

MBELE YANGU:

JINA:              ……………………………….
SAHIHI:          ……………………………….
ANWANI:       ……………………………….
WADHIFA:    ……………………………….

Imesainiwa wa ……………..
………………………………….                               ……………………….
Leo tarehe …… Mwezi
……………………, 2011.

MBELE YANGU:

JINA:              ……………………………….
SAHIHI:          ……………………………….
ANWANI:       ……………………………….
WADHIFA:    ……………………………….





5 comments:

Jeremiah Shauri said...

Simple and clear. Good!

Jeremiah Shauri said...

Simple and clear. Good!

Kalambo, Jr said...

Inapendeza, Ipo poa sana.... Kazi safi, Hongera

anwar said...

mkataba umetulia safi sana

Unknown said...

good one

Post a Comment

Page Views